Social Icons

Wednesday, October 9, 2013


JE WAMFAHAMU VIZURI SNURA MUSHI "MAMAA MAJANGA?

 SOMA HAPA FULL HISTORIA YAKE 

Snura Mushi (Jina lake halisi) alizaliwa tarehe kumi na mbili (12) mwezi wa kwanza (1) mwaka 1984 Jijini Dar es salaam ambako aliweza kukua na kupata elimu yake hapo hapo Dar es salaam. 
 Tofauti na watu wengi wanavyofahamu, kipaji cha mwanadada Snura kilianzia kwenye muziki kabla ya kuigiza na alikuwa na mwimbaji wa taarabu na kundi la “new best star” mwaka 2004. Baada ya hapo alianzisha kundi lake la muziki aliloliita “chanya na hasi” pamoja na vijana wawili mmojawapo akiwa marehemu sharo Milionea kabla hajajiunga rasmi na sanaa ya maigizo. 
 




Kipaji cha mwanadada Snura Kiligunduliwa na mtu aliyefahamika kwa jina la Siasa. 

Ambaye ndiye aliyemfuata na kumshauri kuigiza baada ya kuvutiwa na uzuri na umbo lake ambalo kwa mujibu wa mtu huyo alikuwa na “star look” na angeweza kufanya vizuri kama angejiingiza katika sanaa. Hiyo ilikuwa ni mwaka 2006. Na mwaka huo alipata nafasi ya kuigiza kwenye Filamu ya Mfalme Seuta iliyodirectiwa na Gumbo Kihorota. Baadaye aliweza kucheza movie za Zinduna na Hitimisho.

 Snura alianza kujipatia umaarufu sana kupitia Filamu ya ITUNYAMA, na pia kupitia igizo la Jumba la dhahabu alizofanya akiwa chini ya director Tuesday Kihangala “Mr Chuzi”.

Akizungumzia maisha yake ya ustaa, Snura anasema kuwa huwa anaumizwa sana pale anapoona habari kwenye vyombo vya habari zinazomuhusu ambazo mara nyingi anasema huwa si za kweli.

Katika maisha yake ya kila siku Snura hupendelea sana kukaa ndani na kutazama Filamu mbalimbali kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali.

1 comment: