Baadhi ya Wataalamu wa
kufichua watu wanaojihusisha na vitendo vya ushirikina na uchawi maarufu
KAMCHAPE wamejikuta wakiwa kwenye mikono ya dola baada ya kuendesha
zoezi la kufichua uchawi katika nyumba kadhaa kwenye vijiji mbalimbali
vya manispaa ya Tabora ambapo baadhi ya wananchi walililalamikia zoezi
hilo kwa madai kwamba limekuwa likiwadharirisha baadhi ya watu pamoja na
kujenga chuki ambazo huenda zikasababisha madhara makubwa katika jamii.
Hapa ni baada ya
kufikishwa kituo kikubwa cha Polisi mjini Tabora kwa amri ya Mkuu wa
wilaya ya Tabora Bw.Suleiman Kumchaya ambapo aliwataka kuacha mara moja
zoezi hilo la kufichua wachawi.
No comments:
Post a Comment