POLISI WATIBUA NDOA YA BINTI WA MIAKA 14 HUKO GONGO LA MBOTO..WAWATIA MAHABUSU MAHARUSI WOTE WAWILI!
kwa habari zaidi...
POLISI WATIBUA NDOA YA BINTI WA MIAKA 14 HUKO GONGO LA MBOTO..WAWATIA MAHABUSU MAHARUSI
NDOA iliyokuwa tayari kufungwa na shehe kati ya Hamis Ngaumba (35),
mkazi wa Bangulo, Ulongoni, Gongo la Mboto, Dar na binti wa miaka 14
anayetajwa kwa jina moja la Zubeda, imesambaratishwa na polisi wa Kituo
cha Polisi cha Sitaki-Shari, Dar kutokana na umri wa bi harusi kuwa
mdogo, Amani limeidaka hiyo.
Kizaazaa hicho cha aina yake
kilichovuta hisia za wengi kilitokea saa 10:00 jioni, Jumapili iliyopita
ambapo Shehe Bakari Mgesa wa Msikiti wa Bangulo alikuwa ameanza kutoa
mawaidha ya maandalizi ya kufungisha ndoa hiyo lakini ghafla polisi na
mapaparazi waliingia na shughuli kuishia hapo.
ISHU ILIKUWA HIVImkazi wa Bangulo, Ulongoni, Gongo la Mboto, Dar na binti wa miaka 14
anayetajwa kwa jina moja la Zubeda, imesambaratishwa na polisi wa Kituo
cha Polisi cha Sitaki-Shari, Dar kutokana na umri wa bi harusi kuwa
mdogo, Amani limeidaka hiyo.
Kizaazaa hicho cha aina yake
kilichovuta hisia za wengi kilitokea saa 10:00 jioni, Jumapili iliyopita
ambapo Shehe Bakari Mgesa wa Msikiti wa Bangulo alikuwa ameanza kutoa
mawaidha ya maandalizi ya kufungisha ndoa hiyo lakini ghafla polisi na
mapaparazi waliingia na shughuli kuishia hapo.
Mapema siku ya tukio, msamaria mwema ambaye
hakupendezwa na kitendo hicho alitoa taarifa kwa mapaparazi ambao nao
waliwataarifu polisi wa Kituo cha Polisi Sitaki-Shari na kupewa maafande
kutoka dawati linaloshughulikia unyanyasaji wa kijinsia na kuambatana
nao hadi eneo la tukio.
BREKI YA KWANZA KWA MJUMBE
Kabla ya kufika eneo la tukio, breki
ya kwanza ilikuwa ni kwa mjumbe wa eneo hilo Shina Namba 10, Erasto
Nyakiege ambaye alikiri kusikia taarifa hizo za mtoto kufungishwa ndoa
lakini alizipata muda mfupi kabla polisi na waandishi hao kufika eneo
hilo.
MJUMBE AUNGANA NA POLISI, MAPAPARAZI
Mapaparazi, polisi na mjumbe
huyo waliambatana hadi kwenye nyumba ambayo ilikuwa na shamrashamra za
ndoa hiyo na kumkuta shehe akijiandaa kufungisha huku waalikwa wakiwa
wameshakaa mkao wa kula ‘mnuso’ (pilau).
MSHTUKO WATOKEA, WATU WAKIMBIA
Mshtuko mkubwa ulitokea eneo la
sherehe baada ya watu kuwaona askari, wengine walikimbia kama
wanafukuzwa na simba. Bi harusi yeye alikimbilia chumbani huku bwana
harusi akijichanganya katikati ya wageni waalikwa lakini polisi
walimweka ‘mtukati’.
SHEHE AWA WA KWANZA KUSIMULIA
Akizungumza baada ya kunaswa, Shehe
Bakari alisema ndiyo kwanza alikuwa anajiandaa kwa zoezi la
kuwafungisha ndoa wawili hao lakini kama angebaini kuwa mtoto huyo ana
miaka isiyokidhi vigezo, asingekubali kwa vile hata dini ya Kiislamu
hairuhusu mtoto kuolewa mpaka atimize miaka 18 na kuendelea.
BI HARUSI AWA WA PILI KUWEKA BAYANA
Naye bi harusi, Zubeda ambaye
anaishi na bibi yake aitwaye Bibi Abuu, alieleza kuwa ndoa hiyo ilikuwa
ni kama utani kwani mwanamme huyo alikuwa akimtania tangu akiwa mdogo
akimwambia kuwa akikua atamuoa, hivyo akawa anamuita mchumba lakini
hakuwahi hata siku moja kumtongoza.
MAHARI ILIVYOPELEKWA
Zubeda alisema cha kushangaza siku moja
aliwaona wazazi wa kijana huyo wakipeleka barua ya posa na mahari na
kumkabidhi mjomba na bibi yake kwani baba yake mzazi anaishi Shinyanga
na mama anaishi Tabora, tangu akiwa mdogo anaishi na bibi yake huyo.
“Mimi natamani sana kusoma lakini sina uwezo kwani niliishia darasa la
tatu baada ya wazazi wangu kushindwa kunisomesha ndipo bibi akaja
kunichukua ndiyo maana suala la kuolewa limenitokea tu bila mwenyewe
kupenda. Ilikuwa kama utani lakini wakapokea mahari,” alisema Zubeda
huku akilia kwa uchungu.
BIBI AZUNGUMZA HUKU AKIWA AMELEWA TILALILA
Bibi Abuu alipoona
mambo yameharibika huku akiwa tilalila alikimbilia ndani kulala ambapo
babu wa kufikia wa Zubeda, James alisema ni kweli mjukuu huyo ana miaka
14 na kuongeza kwamba waliopokea mahari ya mtoto huyo kiasi cha shilingi
laki tano na nusu (550,000) ni wajomba pamoja na Bibi Abuu lakini yeye
hajui chochote kuhusiana na ndoa hiyo.
KIUMENI WADAI MAHARI
Baada ya sekeseke hilo, ndugu wa upande wa
mwanamme walikuja juu na kudai mahari yao huku wakitishia kwamba kama
hawatarudishiwa basi wakwe hao watapelekwa polisi kwani hata wao
hawakujua kama huyo anayeolewa ni mtoto wa miaka 14.
WAPELEKWA POLISI
Hata hivyo, polisi waliwazoa ndani ya difenda
bwana harusi, bi harusi na wajomba wawili ambao ndiyo waliopokea mahari
na kwenda kuwaweka nyuma ya nondo kusubiri taratibu za kisheria.
Source: UswazBlog
SHARE NA WASHKAJ WAJANJA
No comments:
Post a Comment