skip to main |
skip to sidebar
Udakuz
STAR TV YAIBUA MAZITO, TUHUMA ZA NGONO CHUO KIKUU DODOMA(UDOM)
Taarifa ya habari ya Star tv ya saa mbili usiku ya tarehe 23/11/2012
imeeleza kuwa wanafunzi wa kike katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)
wanadaiwa kufanya biashara ya ukahaba katika maeneo mbalimbali ya
starehe mjini Dodoma!
Habari hii inasikitisha hasa ukizingatia
umuhimu wa wasomi hawa katika Tanzania na hatari inayoweza kuwapata kama
taarifa hii ina ukweli.
Kama jamii tujiulize, tatizo ni nini mpaka
mtu wa level kama hiyo kuamua kuvaa vichupi na kujiuza kwenye clubs na
sehemu zingine??
CHUO KIKUU cha Dodoma UDOM kinadaiwa kukumbwa na
kashfa ya ngono kufuatia madai kwamba baadhi ya wananafunzi wa kike
wanajihusisha na biashara ya kuuza miili yao kwa lengo la kujikimu
kimaisha.
Tuhuma hizo zimebainika wakati wa mahafali ya tatu ya UDOM
huku takribani wahitimu 6392 wakitunukiwa vyeti,stashahada,shahada za
kwanza,uzamili na shahada za uzamivu.
Chuo Kikuucha Dodoma
ambacho kilianzishwa rasmi mwezi machi mwaka 2007 kimejipatia sifa
kemkekm za kitaaluma licha ya ukweli kwamba bado ni kigeni machoni pa
wengi.
Tuhuma za ngono miongoni mwa wanafunzi wa kike zinadaiwa
kusababishwa na ukata hatua inayowalazimu kutoroka chuoni nyakati za
usiku na kujiunga na baadhi ya wasichana wa mitaani waliokubuhu kwenye
ukahaba maarufu kama machangudoa kwa lengo la kujiuza.
Wakizungumza
na star tv wakati wa mahafali hayo baadhi ya wahitimu wanathibitisha
uwepo wa vitendo hivyo vilivyo kinyume na maadili.
Kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof.Idris Kikula anatoa onyo kali kwa wote watakaobainika.
Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Dodoma Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amenukuliwa kwa
nyakati tofauti akisisitiza suala la maadili chuoni hapo hatua
inayodaiwa kupuuzwa na wanaojihusisha na vitendo hivyo.
du
ReplyDelete